Huduma ya Elimu imegawanyika sehemu tatu.
1. ELIMU MSINGI.
Halmashauri ya wilaya ya Handeni inatoa huduma ya Elimu Msingi ambapo tuna Shule za Msingi 117 na jumla ya wanafunzi 59920 ambapo wavulana ni 29482 na wasichana 30,078.
2. ELIMU SEKONDARI.
Halmashauri ya Wilaya ya Handeni inatoa huduma ya Elimu ya Sekondari ambapo inajumla ya shule za Sekondari 24 ( 23 za Serikali na 1 Binafsi).
3.ELIMU YA WATU WAZIMA.
Halmashauri ya Wilaya ya Handeni inatoa huduma ya Elimu ya Watu wazima wa MEMKWA NA MUKEJA, vituo vya kufundishia vipo 22. Vituo 3 vilivyopo Sindeni,Kabuku na Kwamkono ni vya ufundi stadi. Elimu masafa inawashiriki 7.
Handeni
Postal Address: 355 Handeni
Telephone: 0272977402
Mobile: 0759760156
Email: ded@handenidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa