UTANGULIZI
Halmashauri ya Wilaya ya Handeni ipo kusini mwa mkoa wa Tanga kwa nyuzi za latitude 40 9’ – 60 0’ kusini mwa Ikweta na longitude nyuzi 360 8’ – 380 5’ mashariki mwa ‘‘Greenwich’’. Kwa upande wa Mashariki Wilaya ya Handeni inapakana na Wilaya za Pangani na Muheza, upande wa Kaskazini inapakana na Wilaya za Korogwe na Simanjiro, upande wa Magharibi inapakana nz Wilaya ya Kilindi na upande wa Kusini inapakana na Wilaya ya Bagamoyo.
1.1 ENEO:
Halmashauri ya Wilaya ya Handeni ina eneo la Kilometa za Mraba 6,453 (Ha.637,925.15). Eneo hili ni sawa na asilimia 23.59 ya eneo lote la Mkoa wa Tanga
HALI YA WILAYA (PHYSICAL FEATURES) NA HALI YA HEWA:
Kwa ujumla Halmashauri ya Wilaya HANDENI imegawanyika katika Kanda Kuu mbili nazo ni:-
Ukanda wa Juu (Miinuko na Milima michache):
Ukanda huu unaundwa na miinuko ya milima iliyotawanyika na vilele vya milima ambayo mwinuko wake ni kuanzia meta 600 hadi meta 1,200 kutoka Usawa wa Bahari na umechukua karibu asilimia 75 (4,839.75 km2) ya eneo lote la Halmashauri ya Wilaya ya Handeni. Kiasi cha wastani wa mm800 – mm1000 za mvua hupatikana katika Ukanda huu kwa mwaka.
Ukanda wa Tambarare:
Ukanda huu una mwinuko kati ya Meta 200 hadi Meta 400 kutoka Usawa wa Bahari na wastani wa mvua kwa mwaka ni mm 800 – 1,400. Ukanda umeenea karibu asilimia 25% (1,613.25km2) ya eneo lote la Halmashauri.
Kwa ujumla Wilaya inapata nyuzi joto la 270C mpaka 390C kwa misimu mikuu mitatu ya hali ya hewa:-
Msimu wa joto (Kuanzia mwezi Desemba – Machi)
Msimu wa Mvua (Kuanzia mwezi April – Mei)
Msimu wa Baridi (Juni – Septemba). kwa maelezo zaidi zoma hapa
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa